Karibu katika kitengo cha Mkulima

Mkulima ni kitengo kinachopatikana ndani ya Maktaba ya Taifa ya Sokoine  ya Kilimo (SNAL) iliyoko Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Morogoro. Makusanyo ya machapisho kwa lugha ya kiswahili yanayopatikana ndani ya kitengo; na machapisho mengine yanapatikana kwa njia ya kielektroniki kupitia ghala la Mkulima.  Bonyeza hapa kutafuta machapisho.

Kitengo hiki kilianzishwa mwaka 2016 ikiwa ni marekebisho ya muundo wa SNAL kwa lengo la  kutoa habari na taarifa za kilimo kwa ajili ya matumizi ya wakulima.

Machapisho na taarifa mbalimbali ndani ya kitengo hiki ziko katika lugha ya Kiswahili. Wadau wengine wa sekta ya kilimo kama vile watunga sera na hususani Maafisa Ugani watanufaika na huduma za kitengo hiki katika kupata habari na taarifa kwa ajili ya kusambaza kwa wakulima. Habari na taarifa zinazotolewa na kitengo hiki zimetokana na tafiti mbalimbali zilizofanywa na watalaamu wa SUA na pia kutoka taasisi nyinginezo za utafiti.