Karibu Mkulima Library

Mkulima Library inapatikana ndani ya  Maktaba ya Taifa ya Sokoine  ya Kilimo (SNAL) iliyoko Chuo Kikuu cha Sokoine cha  Kilimo (SUA) mjini Morogoro. Mkulima Library imeanzishwa mwaka 2016 ikiwa ni marekebisho ya muundo wa SNAL kwa lengo la  kutoa habari na taarifa za kilimo kwa ajili ya matumizi ya wakulima hapa Tanzania.

Nyingi ya taarifa ziko katika lugha ya Kiswahili na   kurahisishwa ili ziweze kutumika kiurahisi. Wadau  wengine wa sekta ya kilimo kama vile Maafisa Ugani na watunga sera watafaidika na huduma za kitengo hiki katika kupata habari na taarifa kwa ajili ya kusambaza kwa wakulima.   Habari na taarifa zinazotolewa na   Mkulima Library zimetokana na tafiti mbalimbali zilizofanywa na watalaamu wa SUA na pia kutoka taasisi nyingine za utafiti.